News

Posted On: Apr, 15 2025

Fanyeni kazi kwa uzalendo na uadilifu

News Images

Kaimu Mtendaji Mkuu Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga amewataka watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara kuwa wazalendo, wawajibikaji na waadilifu katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Bodi hiyo.

Kalimbaga ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha ndani cha siku tatu mkoani Morogoro kinacholenga kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, huku akiwataka watumishi hao kushirikiana ili kuleta mabadiliko chanya katika maeneo ya kazi kwa ajili ya kuyafikia malengo waliyojiwekea.

Ameongeza kuwa katika kikao hicho mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo elimu ya utunzaji wa siri za Serikali, elimu kuhusu Afya ya akili pamoja na masuala ya Utumishi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu na Utawala kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara, Aureus Mapunda amesema kikao hicho kitawasaidia watumishi kujikumbusha wajibu wao katika shughuli wanazozifanya mahala pa kazi huku wakitarajia kuwa baada ya kikao hicho utendaji kazi wa Bodi hiyo utaboreka zaidi.