News

Posted On: Mar, 02 2024

Rais Mwinyi Afariki Dunia

News Images

Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kifo cha Mzee Ali Hassan Mwinyi (98), aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mzee Mwinyi amefariki dunia saa 11 jioni Alhamisi Februari 29,2024 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dares Salaam.

"Kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia leo Februari 29 saa 11 jioni katika Hospitali ya Mzena jijini Dares Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya Saratani ya Mapafu.

Mzee Ali Hassan Mwinyi, amekuwa akipatiwa matibabu tangu Novemba mwaka jana huko London, Uingereza na baadaye kurejea nchini na kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena," amesema Dkt. Samia.

Ameongeza kuwa, kutokana na kifo hicho, bendera zitapepea nusu mlingoti kwa siku saba kuanzia Ijumaa, Machi 1, 2024.

Mzee Mwinyi amefariki dunia akiwa na miaka 98 na miezi tisa na siku 21. Sawa na siku 36,091.