Habari

Imewekwa: Sep, 19 2025

RFB Yakagua Barabara ya Singida–Minjingu Km 223.5

News Images


Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara(RFB), wametembelea na kukagua barabara yenye urefu wa kilomita 223.5 ya Singida-Katesh-Dareda-Babati hadi Minjingu, mkoani Singida.

Ziara hiyo imefanyika Septemba 18, 2025 mkoani Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Mussa Natty wakiwa wameambatana na wataalamu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Singida.

Ambapo wajumbe hao wamekagua hali ya barabara ya Singida hadi Minjingu yenye urefu wa kilomita 223.5 ikiwa ni muendelezo wa ziara yao ya kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara tekelezwa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

Hata hivyo Singida umekuwa mkoa wa pili ukitanguliwa na mkoa wa Dodoma kwa wajumbe wa bodi hiyo kutembelea, kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

Wakati bodi hiyo ikiwa mkoani Dodoma,wajumbe walipata fursa ya kukagua na kujionea utekekalezaji wa matengenezo ya barabara ya Dodoma hadi Kitinku yenye urefu wa Km 66.7, uliogharimu kiasi cha milioni 911.

Aidha Bodi ya Mfuko wa Barabara itaendelea na zoezi hilo la ukaguzi katika mkoa wa Arusha, ili kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.