Habari

Imewekwa: Oct, 08 2019

Mfumo wa Tehama kuzilinda barabara

News Images

Bodi ya Mfuko wa Barabara imo mbioni kuzindua mfumo wa Technolojia na Mawasiliano (Tehama) utakaowashirikisha wananchi katika kufuatilia uharibifu na matengenezo ya barabara.

Lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo ni kuwawezesha na kuwashirikisha watumiaji wa barabara kutoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya uharibifu wa miundombinu hiyo.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Barabara, Ndugu Eliud Nyauhenga wakati wa kilele cha sherehe za kuwaaga wajumbe wa mfuko huo na kuwakaribisha wajumbe wapya.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Ndugu Joseph Haule alisema kutokana na umuhimu wa mtandao wa barabara uliopo, mfumo wa teknolojia unaoandaliwa (application software) utasaidia watumiaji wa barabara kutoa taarifa zinazohusu uharibifu wa miundombinu ya barabara kwa nchi nzima.