Karibu
Bodi ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa SHERIA YA BARABARA NA TOZO YA MAFUTA, SURA YA 220. Bodi hii inaundwa na wajumbe tisa, wanne kutoka sekta ya Umma na watano kutoka sekta binafsi.
Wajumbe hao ni Mwenyekiti (kutoka sekta binafsi), Katibu Mkuu - Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu - Wizara ya Fedha na Mipango, Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Mwakilishi wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania, Mwakilishi wa kutoka Hifadhi za Taifa - Tanzania, Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania na Mwakilishi kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania.
Kipindi cha Wajumbe wa kuwa ndani ya Bodi ni Miaka Mitatu (3) unaoendelezwa mara moja tu.